Mara kukatoka uvumi mbinguni kama wa upepo unaovuma na nguvu, ukaijaza nyumba yote, walimokuwa wakikaa. Tena zikaonekana ndimi zilizogawanyika kama za moto, zikawakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho takatifu, wakaanza kusema kwa misemo mingine, kama Roho alivyowapa, watamke.