1
1 Wakorintho 2:9
New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921
SWZZB1921
lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, Wala hayakuingia katika moyo wa kibinadamu, Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Linganisha
Chunguza 1 Wakorintho 2:9
2
1 Wakorintho 2:14
Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Chunguza 1 Wakorintho 2:14
3
1 Wakorintho 2:10
Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho yake. Maana Roho huchunguza yote, hatta mafumbo ya Mungu.
Chunguza 1 Wakorintho 2:10
4
1 Wakorintho 2:12
Na sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho itokayo kwa Mungu, tupate kuyajua tuliyokarimiwa na Mungu.
Chunguza 1 Wakorintho 2:12
5
1 Wakorintho 2:4-5
Na neno langu na kukhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima ya kibinadamu yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho zenye nguvu, imani yenu isiwe katika hekima ya wana Adamu, bali katika nguvu za Mungu.
Chunguza 1 Wakorintho 2:4-5
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video