1
Mathayo 4:4
Neno: Bibilia Takatifu 2025
NENO
Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’”
Linganisha
Chunguza Mathayo 4:4
2
Mathayo 4:10
Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’”
Chunguza Mathayo 4:10
3
Mathayo 4:7
Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”
Chunguza Mathayo 4:7
4
Mathayo 4:1-2
Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi nyikani ili ajaribiwe na ibilisi. Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa.
Chunguza Mathayo 4:1-2
5
Mathayo 4:19-20
Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
Chunguza Mathayo 4:19-20
6
Mathayo 4:17
Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”
Chunguza Mathayo 4:17
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video