Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Efe 1:18

Kumwakisi Yesu
Siku 3
Maisha ya Yesu hapa duniani iliisha na upeo mkubwa: Ufufuo wake, kuonekana baada ya ufufuo, na kupaa mbinguni kimwili. Lakini umewahi kujiuliza nini kilitokea baadaye? Yesu anafanya nini siku hizi? Katika kitabu hiki cha Waefesim Tony Evans anatumia mpango huu mfupi wa usomaji, kutupa kuona kidogo tu jukumu la Yesu sasa na jinsi tunavyopaswa kumwakisi Yeye katika maisha yetu ya kila siku.

Hekima Ya Kiroho
Siku 3
Safari zetu katika maisha mara nyingi zinaweza kuhisi kama barabara nyembamba, yenye hila. Hekima ya kiroho ni njia ya Mungu ya kushughulikia safari yetu ya maisha iliyopinda pinda, na isiyonyoofu. Mpango huu wa siku tatu wa Dk. Tony Evans utakuambia hatua za kufikia na kupata hekima hiyo ya kiroho.

Silaha ya Mungu
Siku 5
Kila siku, vita isiyoonekana inapiganwa kukuzunguka--haionekani, haisikiki, lakini bado unaihisi katika maisha yako yote. Adui wa kishetani aliyejitoa kuleta uharibifu kwa kila kitu muhimu kwako: moyo wako, akili yako, ndoa yako, watoto wako, ndoto zako, hatima yako. Lakini mpango wake wa vita unategemea kukustukiza wakati huna silaha za vita. Kama umechoka kusukumwa na kusitukizwa, somo hili ni kwa ajili yako.

Maombi Hatari
Siku 7
Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, "Dangerous Prayers" yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini.

Siku 21 za Kufurika
Siku 21
Katika siku 21 za kufurika mpango wa YouVersion, Jeremiah Hosford atawachukua wasomaji safari ya majuma 3 ya kujimimina wao kwa wao, kujawa na Roho Mtakatifu, na kuacha mafuriko, na maisha yaliyojaa Roho. Ni wakati wa kuacha kuishi kawaida na kuanza kuishi maisha ya kufurika!

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022
siku 28
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.