Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mdo 4:18

Neno Moja Litakalobadilisha Maisha Yako
Siku 4
NENO MOJA husaidia kurahisisha maisha yako kwa kulenga tu NENO MOJA kwa mwaka mzima. Urahisishaji wa kugundua neno ambalo Mungu amekuwekea inafanya kuwa kichochezi cha maisha yako kubadilika. Vurugu na utata husababisha kuchelewesha na kulemaza, ilhali urahisishaji na lengo husababisha mafanikio na uwazi. Ibada hii ya siku nne inakuonyesha jinsi ya kupata kiini cha nia yako kwa maono ya neno moja kwa mwaka.

Utiifu
Wiki 2
Yesu mwenyewe alisema ambaye yeyote anaye mupenda atatii mafundisho Yake. Haijalishi gharama yake kwa kila mutu, utiifu wetu ndio wa muhimu kwa Mungu. "Utiifu" Mpango wa usomaji inachukua jinsi maandiko yanavyo sema kuhusu utiifu: Namna gani kulinda musimamo ya uadilifu, jukumu ya rehema, namna gani utiifu hutufanya huru na hubariki maisha yetu, na kadhalika.

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume
Siku 20
BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023
Siku 30
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.