Yoeli 3

3
Yawe atashusha Roho wake
1Kisha mambo hayo
nitashusha Roho wangu juu ya watu wote.
Watoto wenu wanaume na wabinti watatabiri,
wazee wenu wataota ndoto,
na vijana wenu wataona maono. #Ang. Mdo 2.17-21
2Hata juu ya watumishi wanaume na wanawake,
nitashusha Roho wangu wakati huo.
3Nitafanya kitambulisho cha ajabu mbinguni na katika dunia;
kutakuwa damu, moto na minara ya moshi.
4Jua litatiwa giza,
na mwezi utakuwa kama damu,
mbele ya kutimia kwa siku ya Yawe,
siku inayokuwa kubwa na ya kutisha. #Ang. Mat 24.29; Mk 13.24-25; Lk 21.25; Ufu 6.12-13
5Halafu, watu wote watakaoomba kwa jina la Yawe wataokolewa.
Katika mulima Sayuni na Yerusalema,
kutakuwa watu watakaoponyoka,
kama vile Yawe alivyosema:
wale aliowachagua watabaki wazima. #Ang. Rom 10.13

اکنون انتخاب شده:

Yoeli 3: SWC02

های‌لایت

کپی

مقایسه

به اشتراک گذاشتن

None

می خواهید نکات برجسته خود را در همه دستگاه های خود ذخیره کنید؟ برای ورودثبت نام کنید یا اگر ثبت نام کرده اید وارد شوید