1
Warumi 14:17-18
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
TKU
Maisha katika ufalme wa Mungu siyo juu ya kile tunachokula na kunywa. Ufalme wa Mungu ni juu ya njia sahihi ya kuishi, amani na furaha. Vyote hii vinatoka kwa Roho Mtakatifu. Yeyote anayemtumikia Kristo kwa kuishi namna hii anampendeza Mungu na ataheshimiwa na wengine.
Compara
Explorar Warumi 14:17-18
2
Warumi 14:8
Kama tukiishi, tunaishi kwa ajili ya Bwana. Na kama tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Hivyo kuishi au kufa, sisi ni mali ya Bwana.
Explorar Warumi 14:8
3
Warumi 14:19
Hivyo tujitahidi kwa kadri tuwezavyo kufanya kile kinacholeta amani. Tufanye kile kitakachomsaidia kila mtu kujengeka kiimani.
Explorar Warumi 14:19
4
Warumi 14:13
Hivyo tuache kuhukumiana sisi kwa sisi. Tuamue kutokufanya kitu ambacho kitasababisha matatizo kwa kaka au dada au kuathiri imani zao.
Explorar Warumi 14:13
5
Warumi 14:11-12
Ndiyo, Maandiko yanasema, “‘Hakika kama niishivyo’, asema Bwana, ‘kila mtu atapiga magoti mbele zangu, na kila mtu atasema kuwa mimi ni Mungu.’” Hivyo kila mmoja wetu ataeleza kuhusu matendo yake mbele za Mungu.
Explorar Warumi 14:11-12
6
Warumi 14:1
Iweni tayari kuwakubali wenye mashaka kuhusu yale ambayo waamini wanaweza kufanya. Tena msibishane nao kuhusu mawazo yao tofauti.
Explorar Warumi 14:1
7
Warumi 14:4
Huwezi kuwahukumu watumishi wa mtu mwingine. Hilo linamhusu bwana wao mwenyewe ikiwa watafaulu au watashindwa. Na watakubaliwa, kwa sababu Bwana yuko tayari kuwafanya wafaulu.
Explorar Warumi 14:4