Soma Biblia Kila Siku Mei 2021预览

Mara akawalazimisha wanafunzi wake (m.45). Kwa nini? Jana tuliona kuwa Yesu alitaka wapumzike baada ya kufanya kazi nyingi, lakini haikuwezekana kutokana na mkutano mkubwa uliowafuata. Hata hivyo baada ya kumaliza kusaidia mkutano huo, Yesu alizidi kusisitiza ni lazima wapumzike ili wapate nguvu mpya kimwili na kiroho. Vivyo hivyo kwa Yesu mwenyewe. Akaenda zake mlimani kuomba (m.46). Ndugu msomaji uliye mtumishi wa Bwana, tafadhali uzingatie sana fundisho hili la Yesu, usije ukadhoofika kimwili na kiroho na kumpa Shetani nafasi!