Soma Biblia Kila Siku 06/2020预览

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

30天中的第19天

Lengo la mfano huu wa mamba na nguvu zake laonekana katika m.11: "Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu". Nguvu za mamba zashuhudia uwezo mkuu wa Mungu aliyemwumba. Mungu amejitosheleza kwa vitu vyote. Sisi twavuna kutoka kwake sehemu ndogo ya vipawa vyake vifanyike msaada kwetu, watoto wetu na ndugu zetu. Zab 125:1 yatia muhuri ukweli huu: Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.. Kila aishiye kwa tumaini la kuwezeshwa na Bwana hataishiwa matumaini wala kujuta. Mtegemee Mungu, mweza wa vyote na mpaji wa vyote.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More