Soma Biblia Kila Siku 03/2020预览

Daudi hakupata kuwa mfalme juu ya Israeli yote kwa mara moja. Akawa kwanza mfalme juu ya kabila lake tu (Wayuda). Kuna sababu mbili. 1. Abneri, kamanda wa jeshi la Sauli, alikuwa shujaa na mwenye mamlaka sana (kwa mfano imeandikwa katika m.9 kwamba Abneri akamweka [mwana wa Sauli] awe mfalme). Tena ni ndugu yake Sauli kiukoo. 2. Kawaida ni kwamba mtoto wa mfalme anaurithi ufalme mara mfalme akifa. Hivyo Ishboshethi akawa mfalme. –Daudi alifanyaje? Daudi akauliza kwa Bwana (m.1), maana alikuwa amejiweka kabisa chini ya uongozi wa Bwana! Alimtegemea kwa kilajambo. Nasi tuige mfano wake!