Soma Biblia Kila Siku 03/2020预览

Wakuu wa dini walimpeleka Yesu kwa mtawala wa mataifa, wakitaka tamko la hukumu ya kiserikali. Liwali hakuona hatia kwa Yesu, na alitangaza wazi kutojihusisha na kifo cha Yesu. Lakini watu wa taifa lake Yesu na viongozi wa dini waliamua ni lazima Yesu afe. Ndiyo, ni huzuni kwamba Yesu alikuja kwake, lakini walio wake hawakumpokea(Yn 1:11). Kumbuka pia, Yesu alivyofundisha: Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni (Mt 5:20). Wakristo, twaitwa tuwe watu wa haki katika matendo yetu na mienendo yetu.