Soma Biblia Kila Siku 03/2020预览

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

31天中的第7天

Yoabu alikuwa anatoa maneno ya udhuru kwa Daudi kwamba Abneri alikuja ili kudanganya: Wewe wamjua Abneri, mwana wa Neri, ya kuwa alikuja ili kukudanganya, apate kujua kutoka kwako, na kuingia kwako, akajue yote uyatendayo(m.25). Ila sababu yake ya kweli ya kumwua ni kwamba Abneri alikuwa amemwua Asaheli, ndugu yake Yoabu (m.27, 30). Makosa ya Yoabu ni mawili. 1. Kumwua Abneri bila ruhusa kutoka kwa mfalme (m.26: Daudi alikuwa hana habari. Katika m.28 Daudi mwenyewe anathibitisha hiyo). 2. Alimwua kwa kutumia mtego. Haistahili kwa mwanajeshi (taz. m.34 Daudi anapomwomboleza Abneri, akisema, Aangukavyo mtu mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka). Asaheli alikuwa mtoto wa Seruja, dada yake Daudi (m.39; 1 Nya 2:16). Hata hivyo maombolezo ya Daudi yalitoka kweli moyoni (m.37: Wakajua watu wote, na Israeli wote, siku ile, ya kuwa si nia ya mfalme kwamba auawe Abneri)! Daudi hakuwa na mawazo mafupi!

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More