Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako,
Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.
Wakipita kati ya bonde la Vilio,
Hulifanya kuwa chemchemi,
Naam, mvua ya vuli hulivika baraka
Huendelea toka nguvu hata nguvu,
Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.