Psalms 84:10-12

Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu. Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu. Ee BWANA wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.
Zab 84:10-12