Psalm 54:1-7

Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu. Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu. Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao. Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia; Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu. Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako. Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema. Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu.
Zab 54:1-7