Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu;
Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.
Sauti ya BWANA i juu ya maji;
Mungu wa utukufu alipiga radi;
BWANA yu juu ya maji mengi.
Sauti ya BWANA ina nguvu;
Sauti ya BWANA ina adhama