Wewe, BWANA, nguvu zangu, nakupenda sana;
BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu,
Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia,
Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa,
Hivyo nitaokoka na adui zangu.