Msikilize baba yako aliyekuzaa,
Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
Inunue kweli, wala usiiuze;
Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu.
Baba yake mwenye haki atashangilia;
Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia.
Na wafurahi baba yako na mama yako;
Na afurahi aliyekuzaa.