Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu;
Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.
Kiburi hutangulia uangamivu;
Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini,
Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.