Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Proverbs 11:1-31

Mit 11:1-31 - Mizani ya hadaa ni chukizo kwa BWANA;
Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.
Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu;
Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.
Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza
Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.
Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu;
Bali haki huokoa na mauti.
Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake;
Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake.
Haki yao wenye haki itawaokoa;
Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.
Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea;
Na matumaini ya uovu huangamia.
Mwenye haki huokolewa katika dhiki,
Na mtu mwovu ataiingia badala yake.
Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake;
Bali wenye haki watapona kwa maarifa.
Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi;
Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele.
Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki;
Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.
Asiye na akili humdharau mwenziwe;
Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
Mwenye kitango akisingizia hufunua siri;
Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.
Pasipo mashauri taifa huanguka;
Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;
Achukiaye mambo ya dhamana yu salama.
Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima;
Na watu wakali hushika mali siku zote.
Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake;
Aliye mkali hujisumbua mwili wake.
Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu;
Apandaye haki ana thawabu ya hakika.
Haki huelekea uzima;
Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe.
Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa BWANA;
Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza.
Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu;
Bali wazao wa wenye haki wataokoka.
Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe,
Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.
Haja ya mwenye haki ni mema tu;
Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu.
Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi;
Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.
Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa;
Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.
Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani;
Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake.
Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili;
Atafutaye madhara, hayo yatamjia.
Azitegemeaye mali zake ataanguka;
Mwenye haki atasitawi kama jani.
Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo;
Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili.
Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima;
Na mwenye hekima huvuta roho za watu.
Tazama, mwenye haki atalipwa duniani;
Basi mwovu na mkosaji si mara nyingi zaidi?

Mizani ya hadaa ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe. Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake. Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa. Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele. Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu. Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu. Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama. Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote. Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake. Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu; Apandaye haki ana thawabu ya hakika. Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe. Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa BWANA; Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza. Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazao wa wenye haki wataokoka. Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili. Haja ya mwenye haki ni mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu. Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe. Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake. Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia. Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani. Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili. Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu. Tazama, mwenye haki atalipwa duniani; Basi mwovu na mkosaji si mara nyingi zaidi?

Mit 11:1-31