Tafuta matokeo ya: we all are sheep gone astray
Isa 53:6 (SUV)
Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
1 Pet 2:25 (SUV)
Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.
Lk 15:4 (SUV)
Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?
Zab 23:1 (SUV)
BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
Zab 23:2 (SUV)
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
Zab 23:3 (SUV)
Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Zab 23:4 (SUV)
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Zab 23:5 (SUV)
Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
Zab 23:6 (SUV)
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Yn 10:11 (SUV)
Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
Yn 10:14 (SUV)
Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;
Yer 50:6 (SUV)
Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika.
Ebr 13:20 (SUV)
Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,
1 Pet 5:4 (SUV)
Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.