Sefania 2:7,9
Sefania 2:7 Biblia Habari Njema (BHN)
Nchi ya pwani itamilikiwa na mabaki ya ukoo wa Yuda. Watachunga mifugo yao huko. Nyumba za mji wa Ashkeloni zitakuwa mahali pao pa kulala. Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wao atawakumbuka na kuwarudishia hali yao njema.
Sefania 2:9 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa hiyo, niishivyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, mimi Mungu wa Israeli, Moabu itakuwa kama Sodoma na Amoni itakuwa kama Gomora. Nchi zake zitakuwa za viwavi na mashimo ya chumvi, zitakuwa ukiwa milele. Watu wangu watakaobaki wataziteka nyara, watu wa taifa langu waliosalia watazimiliki.”
Sefania 2:7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watachunga makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana BWANA, Mungu wao, atawajia na kuwarudisha wafungwa wao.
Sefania 2:9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.
Sefania 2:7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watalisha makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana BWANA, Mungu wao, atawajilia na kuwarudisha wafungwa wao.
Sef 2:9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.
Sefania 2:7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda, hapo watapata malisho. Wakati wa jioni watajilaza chini katika nyumba za Ashkeloni. BWANA Mungu wao atawatunza, naye atawarudishia wafungwa wao.
Sefania 2:9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hakika, kama niishivyo,” asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, “hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, Waamoni kama Gomora: mahali pa magugu na mashimo ya chumvi, nchi ya ukiwa milele. Mabaki ya watu wangu watawateka nyara; mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”