Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Sefania 2:4-15

Sefania 2:4-15 Biblia Habari Njema (BHN)

Mji wa Gaza utahamwa, Ashkeloni utakuwa tupu. Wakazi wa Ashdodi watatimuliwa mchana, na wale wa Ekroni watang'olewa. Ole wenu wakazi wa nchi za pwani, watu mnaoishi huko Krete! Mwenyezi-Mungu ametamka dhidi yenu enyi wakazi wa Kanaani, nchi ya Filistia: Mimi nitawaangamiza asibaki hata mkazi mmoja! Nanyi nchi za pwani mtafanywa kuwa malisho; mtakuwa vibanda vya wachungaji na mazizi ya kondoo. Nchi ya pwani itamilikiwa na mabaki ya ukoo wa Yuda. Watachunga mifugo yao huko. Nyumba za mji wa Ashkeloni zitakuwa mahali pao pa kulala. Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wao atawakumbuka na kuwarudishia hali yao njema. “Nimeyasikia masuto ya Moabu na dhihaka za Waamoni; jinsi walivyowasuta watu wangu, na kujigamba kuiteka nchi yao. Kwa hiyo, niishivyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, mimi Mungu wa Israeli, Moabu itakuwa kama Sodoma na Amoni itakuwa kama Gomora. Nchi zake zitakuwa za viwavi na mashimo ya chumvi, zitakuwa ukiwa milele. Watu wangu watakaobaki wataziteka nyara, watu wa taifa langu waliosalia watazimiliki.” Hayo yatakuwa malipo ya kiburi chao, kwa sababu waliwadhihaki na kujigamba dhidi ya watu wa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mwenyezi-Mungu atakuwa wa kutisha dhidi yao; miungu yote ya dunia ataikondesha. Mataifa yote duniani yatamsujudia; kila taifa katika mahali pake. Nanyi watu wa Kushi pia mtauawa kwa upanga wake. Mwenyezi-Mungu atanyosha mkono wake kaskazini, na kuiangamiza nchi ya Ashuru. Ataufanya mji wa Ninewi kuwa ukiwa, kuwa mahali pakavu kama jangwa. Makundi ya mifugo yatalala humo, kadhalika kila mnyama wa porini. Tai na yangeyange na korongo wataishi juu ya nguzo zake, bundi watalia kwenye madirisha yake, kunguru watalia kwenye vizingiti, maana nyumba zake za mierezi zitakuwa tupu. Je, huu ndio mji uliojivuna na kuishi kwa usalama, mji uliojisemea, “Ni mimi tu, hakuna mwingine!” Jinsi gani umekuwa mtupu na makao ya wanyama wa mwituni! Kila apitaye karibu atauzomea na kuudharau.

Shirikisha
Soma Sefania 2

Sefania 2:4-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Kwa kuwa Gaza utaachwa, na Ashkeloni utakuwa ukiwa; wataufukuzia mbali Ashdodi wakati wa adhuhuri, na Ekroni utang'olewa. Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la BWANA liko juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako. Na hiyo nchi ya pwani itakuwa malisho, yenye vibanda vya wachungaji, na mazizi ya makundi ya kondoo. Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watachunga makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana BWANA, Mungu wao, atawajia na kuwarudisha wafungwa wao. Mimi nimeyasikia masuto ya Moabu, na dhihaka za wana wa Amoni, ambazo kwa hizo wamewatukana watu wangu, na kujitukuza juu ya mpaka wao. 21:28-32; 25:1-11; Amo 1:13-15 Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi. Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa BWANA wa majeshi, na kujitukuza juu yao. BWANA atakuwa wa kutisha sana kwao; kwa maana atawaua kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa. Na ninyi Wakushi pia, mtauawa kwa upanga wangu. Naye atanyosha mkono wake juu ya upande wa kaskazini, na kuiangamiza Ashuru; naye ataufanya Ninawi kuwa ukiwa, kuwa mahali pakavu kama jangwa. Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; bundi na kunguru watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi. Huu ndio mji ule wa furaha, Uliokaa salama, Uliosema moyoni mwake, Mimi niko, Wala hapana mwingine ila mimi. Jinsi ulivyokuwa ukiwa, Mahali pa kulala pa wanyama wa bara! Kila mtu apitaye atazomea, Na kutikisa mkono wake.

Shirikisha
Soma Sefania 2

Sefania 2:4-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Kwa kuwa Gaza utaachwa, na Ashkeloni utakuwa ukiwa; wataufukuzia mbali Ashdodi wakati wa adhuhuri, na Ekroni utang’olewa. Amo 1:6-8; Zek 9:5-7 Ole wao wakaao karibu na pwani ya bahari, taifa la Wakerethi! Neno la BWANA li juu yenu, Ee Kanaani, nchi ya Wafilisti; mimi nitakuangamiza, asibaki mtu akaaye kwako. Na hiyo nchi ya pwani itakuwa malisho, yenye vibanda vya wachungaji, na mazizi ya makundi ya kondoo. Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watalisha makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana BWANA, Mungu wao, atawajilia na kuwarudisha wafungwa wao. Mimi nimeyasikia matukano ya Moabu, na dhihaka za wana wa Amoni, ambazo kwa hizo wamewatukana watu wangu, na kujitukuza juu ya mpaka wao. 21:28-32; 25:1-11; Amo 1:13-15 Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi. Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa BWANA wa majeshi, na kujitukuza juu yao. BWANA atakuwa mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawafisha kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa. Na ninyi Wakushi pia, mtauawa kwa upanga wangu. Naye atanyosha mkono wake juu ya upande wa kaskazini, na kuiangamiza Ashuru; naye ataufanya Ninawi kuwa ukiwa, kuwa mahali pakavu kama jangwa. Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; mwari-nyuni na nungu watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi. Huu ndio mji ule wa furaha, Uliokaa pasipo kufikiri, Uliosema moyoni mwake, Mimi niko, Wala hapana mwingine ila mimi. Jinsi ulivyokuwa ukiwa, Mahali pa kulala pa wanyama wa bara! Kila mtu apitaye atazomea, Na kutikisa mkono wake.

Shirikisha
Soma Sefania 2

Sefania 2:4-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Gaza utaachwa na Ashkeloni utaachwa magofu. Wakati wa adhuhuri Ashdodi utaachwa mtupu, na Ekroni utangʼolewa. Ole wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari, enyi Wakerethi; neno la BWANA liko dhidi yenu, ee Kanaani, nchi ya Wafilisti. “Mimi nitawaangamiza, na hakuna atakayebaki.” Nchi iliyo karibu na bahari itakuwa malisho yenye visima vya wachungaji, na mazizi ya kondoo. Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda, hapo watapata malisho. Wakati wa jioni watajilaza chini katika nyumba za Ashkeloni. BWANA Mungu wao atawatunza, naye atawarudishia wafungwa wao. “Nimeyasikia matukano ya Moabu nazo dhihaka za Waamoni, ambao waliwatukana watu wangu na kutoa vitisho dhidi ya nchi yao. Hakika, kama niishivyo,” asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, “hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, Waamoni kama Gomora: mahali pa magugu na mashimo ya chumvi, nchi ya ukiwa milele. Mabaki ya watu wangu watawateka nyara; mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.” Hiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi chao, kwa kutukana na kudhihaki watu wa BWANA wa majeshi. BWANA atakuwa wa kuhofisha kwao atakapoangamiza miungu yote ya nchi. Mataifa katika kila pwani yatamwabudu, kila moja katika nchi yake. “Ninyi pia, ee Wakushi, mtauawa kwa upanga wangu.” Mungu atanyoosha mkono wake dhidi ya kaskazini na kuangamiza Waashuru, akiiacha Ninawi ukiwa na pakame kama jangwa. Makundi ya kondoo na ngʼombe yatajilaza pale, viumbe vya kila aina. Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba wataishi juu ya nguzo zake. Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani, kifusi kitakuwa milangoni, boriti za mwerezi zitaachwa wazi. Huu ndio mji uliotukuka na kuishi kwa furaha wakijisikia salama. Ulisema moyoni mwako, “Mimi ndimi, na wala hapana mwingine ila mimi.” Jinsi gani umekuwa gofu, mahali pa kulala wanyama pori! Wote wanaopita kando yake wanauzomea na kutikisa mkono kwa dharau.

Shirikisha
Soma Sefania 2