Sefania 2:1-3
Sefania 2:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilo na haya; kabla haijazaa hiyo amri, kabla haijapita siku ile kama makapi, kabla haijawajilia hasira kali ya BWANA, kabla haijawajilia siku ya hasira ya BWANA. Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.
Sefania 2:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Kusanyikeni, kusanyikeni enyi taifa la watu wasio na aibu, kabla hamjapeperushwa mbali kama makapi, kabla haijawajia siku ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu, kabla haijawajia siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu. Mtafuteni Mwenyezi-Mungu enyi wanyenyekevu wote nchini, enyi mnaozitii amri zake. Tafuteni uadilifu, tafuteni unyenyekevu; labda mtaiepa siku ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.
Sefania 2:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilo na haya; kabla haijatolewa hiyo amri, kabla siku ile haijapita kama makapi, kabla haijawajia hasira kali ya BWANA, kabla haijawajia siku ya hasira ya BWANA. Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.
Sefania 2:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jikusanyeni, naam, jikusanyeni, Ee taifa lisilo na haya; kabla haijazaa hiyo amri, kabla haijapita siku ile kama makapi, kabla haijawajilia hasira kali ya BWANA, kabla haijawajilia siku ya hasira ya BWANA. Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.
Sefania 2:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kusanyikeni pamoja, kusanyikeni pamoja, enyi taifa lisilo na aibu, kabla wakati ulioamriwa haujafika na siku ile inayopeperusha kama makapi, kabla hasira kali ya BWANA haijaja juu yenu, kabla siku ya ghadhabu ya BWANA haijaja juu yenu. Mtafuteni BWANA, enyi nyote wanyenyekevu wa nchi, ninyi ambao hufanya lile analoamuru. Tafuteni haki, tafuteni unyenyekevu; labda mtahifadhiwa siku ya hasira ya BWANA.