Sefania 1:2-5
Sefania 1:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema: “Nitavifagilia mbali viumbe vyote duniani: Wanadamu, wanyama, ndege wa angani na samaki wa baharini; vyote nitaviangamiza. Waovu nitawaangamiza kabisa; wanadamu nitawafagilia mbali duniani. Nitaunyosha mkono wangu dhidi ya nchi ya Yuda, kadhalika na wakazi wote wa mji wa Yerusalemu. Nitaangamiza mabaki yote ya Baali kutoka nchi hii, na hakuna atakayetambua jina lao. Nitawaangamiza wote wanaosujudu juu ya paa, wakiabudu jeshi la mbinguni. Nitawaangamiza wale wanaoniabudu na kuapa kwa jina langu, hali wanaapa pia kwa jina la mungu Milkomu.
Sefania 1:2-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nitavikomesha kabisa vitu vyote, visionekane juu ya uso wa nchi, asema BWANA. Nitamkomesha mwanadamu na mnyama; nitakomesha ndege wa angani, na samaki wa baharini, na hayo yakwazayo pamoja na waovu; nami nitamkatilia mbali mwanadamu, asionekane juu ya uso wa nchi, asema BWANA. Nami nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani; na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya madari ya nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa BWANA na kuapa pia kwa Milkomu
Sefania 1:2-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nitavikomesha kabisa vitu vyote, visionekane juu ya uso wa nchi, asema BWANA. Nitamkomesha mwanadamu na mnyama; nitakomesha ndege wa angani, na samaki wa baharini, na hayo makwazo pamoja na wabaya; nami nitamkatilia mbali mwanadamu, asionekane juu ya uso wa nchi, asema BWANA. Nami nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani; na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa BWANA na kuapa pia kwa Malkamu
Sefania 1:2-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA asema, “Nitafagia kila kitu kutoka uso wa dunia. Nitafagilia mbali watu na wanyama; nitafagilia mbali ndege wa angani na samaki wa baharini. Wafanyao maovu watapata tu kokoto, nami nitamkatilia mbali mwanadamu atoke katika dunia,” asema BWANA. “Nitaiadhibu Yuda na wote wanaoishi Yerusalemu. Kutoka mahali hapa nitakatilia mbali kila mabaki ya Baali, majina ya wapagani na makuhani waabuduo sanamu: wale ambao husujudu juu ya mapaa kuabudu jeshi la vitu vya angani, wale ambao husujudu na kuapa kwa BWANA na ambao pia huapa kwa Malkamu