Sefania 1:14-16
Sefania 1:14-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Ile siku kubwa ya Mwenyezi-Mungu imekaribia, iko karibu na inakuja mbio. Mlio wa siku ya Mwenyezi-Mungu ni wa uchungu; hapo, shujaa atalia kwa sauti. Siku hiyo itakuwa siku ya ghadhabu, ni siku ya dhiki na uchungu, siku ya giza na huzuni; siku ya uharibifu na maangamizi, siku ya mawingu na giza nene. Siku hiyo ni ya mlio wa tarumbeta ya vita, dhidi ya miji yenye ngome na kuta ndefu.
Sefania 1:14-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya BWANA; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko! Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu, Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Na juu ya minara mirefu.
Sefania 1:14-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya BWANA; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko! Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu, Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.
Sefania 1:14-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Siku kubwa ya BWANA iko karibu: iko karibu na inakuja haraka. Sikilizeni! Kilio katika siku ya BWANA kitakuwa chungu. Shujaa atapiga ukelele wa vita huko. Siku ile ni siku ya ghadhabu, siku ya fadhaa na dhiki, siku ya uharibifu na ukiwa, siku ya giza na utusitusi, siku ya mawingu na giza nene, siku ya tarumbeta na kelele za vita dhidi ya miji yenye ngome, na dhidi ya minara mirefu.