Zekaria 9:9-10
Zekaria 9:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Shangilieni sana enyi watu wa Siyoni! Paazeni sauti, enyi watu wa Yerusalemu! Tazama, mfalme wenu anawajieni, anakuja kwa shangwe na ushindi! Ni mpole, amepanda punda, mwanapunda, mtoto wa punda. Atatokomeza magari ya vita nchini Efraimu, na farasi wa vita kutoka mjini Yerusalemu; pinde za vita zitavunjiliwa mbali. Naye ataleta amani miongoni mwa mataifa; utawala wake utaenea toka bahari hata bahari, toka mto Eufrate hata miisho ya dunia.
Zekaria 9:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda. Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiria mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.
Zekaria 9:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda. Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiri mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.
Zekaria 9:9-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Shangilia sana, ee Binti Sayuni! Piga kelele, Binti Yerusalemu! Tazama, Mfalme wako anakuja kwako, ni mwenye haki, naye ana wokovu, ni mpole, naye amepanda punda, mwana-punda, mtoto wa punda. Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu na farasi wa vita kutoka Yerusalemu, nao upinde wa vita utavunjwa. Atatangaza amani kwa mataifa. Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari, na kutoka Mto hadi mwisho wa dunia.