Zekaria 4:11-14
Zekaria 4:11-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Nami nikazidi kuuliza, “Je, hiyo miti miwili ya mizeituni iliyo upande wa kulia na wa kushoto wa kinara, inamaanisha nini? Na hayo matawi mawili pembeni mwa mirija miwili ya dhahabu ambamo mafuta ya mizeituni hutiririkia, yanamaanisha nini?” Naye akaniambia, “Je, hujui?” Nami nikamjibu, “La, sijui Bwana!” Hapo akaniambia, “Matawi haya ndio wale watu wawili waliowekwa wakfu kwa mafuta wamtumikie Bwana wa ulimwengu wote.”
Zekaria 4:11-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo nikajibu, nikamwambia, Ni nini mizeituni hii miwili iliyo upande wa kulia wa kinara cha taa kile na upande wake wa kushoto? Na kwa mara ya pili, nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yao? Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili watiwa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.
Zekaria 4:11-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo nikajibu, nikamwambia, Ni nini mizeituni hii miwili iliyo upande wa kuume wa kinara cha taa kile na upande wake wa kushoto? Nami nikajibu mara ya pili, nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yao? Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.
Zekaria 4:11-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha nikamuuliza yule malaika, “Hii mizeituni miwili iliyo upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni nini?” Tena nikamuuliza, “Haya matawi mawili ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni nini?” Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?” Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.” Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.”