Zekaria 13:8-9
Zekaria 13:8-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Theluthi mbili za watu katika nchi zitaangamizwa; ni theluthi moja tu itakayosalimika. Theluthi hiyo moja itakayosalia, nitaijaribu na kuitakasa, kama mtu asafishavyo fedha, naam, kama ijaribiwavyo dhahabu. Hapo wao wataniomba mimi, nami nitawajibu. Nitasema, ‘Hawa ni watu wangu’, nao watasema, ‘Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu wetu.’”
Zekaria 13:8-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema BWANA; lakini fungu la tatu litabaki humo. Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.
Zekaria 13:8-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema BWANA; lakini fungu la tatu litabaki humo. Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.
Zekaria 13:8-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
katika nchi yote,” asema BWANA, “theluthi mbili watapigwa na kuangamia; hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake. Hii theluthi moja nitaileta katika moto; nitawasafisha kama fedha isafishwavyo na kuwajaribu kama dhahabu. Wataliitia Jina langu nami nitawajibu; nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ nao watasema, ‘BWANA ni Mungu wetu.’ ”