Zekaria 11:4-5
Zekaria 11:4-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, alisema hivi: “Jifanye mchungaji wa kondoo waendao kuchinjwa. Wanunuzi wao wanawachinja lakini hawaadhibiwi; na wauzaji wao wanasema, ‘Na ashukuriwe Mwenyezi-Mungu! Sasa tumetajirika’. Hata wachungaji wenyewe hawawaonei huruma.
Zekaria 11:4-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, Mungu wangu, alisema hivi, Lilishe kundi la machinjo, ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe BWANA, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.
Zekaria 11:4-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, Mungu wangu, alisema hivi, Lilishe kundi la machinjo, ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe BWANA, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.
Zekaria 11:4-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hili ndilo asemalo BWANA Mungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa. Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘Ahimidiwe BWANA, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.