Wimbo Ulio Bora 8:5-7
Wimbo Ulio Bora 8:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Ni nani huyu ajaye kutoka mbugani, huku anamwegemea mpenzi wake? Chini ya mtofaa, mimi nilikuamsha, pale ambapo mama yako aliona uchungu, naam, pale ambapo mama yako alikuzaa. Nipige kama mhuri moyoni mwako, naam, kama mhuri mikononi mwako. Maana pendo lina nguvu kama kifo, wivu nao ni mkatili kama kaburi. Mlipuko wake ni kama mlipuko wa moto, huwaka kama mwali wa moto. Maji mengi hayawezi kamwe kulizima, mafuriko hayawezi kulizamisha. Mtu akijaribu kununua pendo, akalitolea mali yake yote, atakachopata ni dharau tupu.
Wimbo Ulio Bora 8:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Akimtegemea mpendwa wake? Nilikuamsha chini ya huo mpera; Huko mama yako alikuonea uchungu, Aliona uchungu aliyekuzaa. Nitie kama mhuri moyoni mwako, Kama mhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu. Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa.
Wimbo Ulio Bora 8:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Akimtegemea mpendwa wake? Nalikuamsha chini ya huo mpera; Huko mama yako alikuonea utungu, Aliona utungu aliyekuzaa. Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu. Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa.
Wimbo Ulio Bora 8:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani akimwegemea mpenzi wake? Nilikuamsha chini ya mtofaa, huko mama yako alipotunga mimba yako, huko yeye alipata uchungu akakuzaa. Nitie kama muhuri moyoni mwako, kama muhuri kwenye mkono wako; kwa maana upendo una nguvu kama mauti, wivu wake ni mkatili kama Kuzimu. Unachoma kama mwali wa moto, kama mwali mkubwa wa moto wa BWANA hasa. Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, mito haiwezi kuugharikisha. Kama mtu angetoa mali yote ya nyumbani mwake kwa ajili ya upendo, angedharauliwa kabisa.