Wimbo Ulio Bora 7:11-13
Wimbo Ulio Bora 7:11-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Njoo ewe mpenzi wangu, twende mashambani, twende zetu tukalale huko vijijini. Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu, tukaone kama imeanza kuchipua, na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua, pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua. Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu. Harufu nzuri ya tunguja imejaa hewani karibu na milango yetu kuna kila aina ya matunda bora, yote mapya na ya siku za nyuma, ambayo nimekuwekea wewe mpenzi wangu.
Wimbo Ulio Bora 7:11-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji. Twende mapema hadi mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabibu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa upendo wangu. Mitunguja hutoa harufu yake; Juu ya milango yetu yako matunda mazuri, Mapya na ya kale, ya kila namna, Niliyokuwekea, mpendwa wangu.
Wimbo Ulio Bora 7:11-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji. Twende mapema hata mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabihu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa pambaja zangu. Mitunguja hutoa harufu yake; Juu ya milango yetu yako matunda mazuri, Mapya na ya kale, ya kila namna, Niliyokuwekea, mpendwa wangu.
Wimbo Ulio Bora 7:11-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani, twende tukalale huko vijijini. Hebu na twende mapema katika mashamba ya mizabibu tuone kama mizabibu imechipua, kama maua yake yamefunguka, na kama mikomamanga imetoa maua: huko nitakupa penzi langu. Mitunguja hutoa harufu zake nzuri, kwenye milango yetu kuna matunda mazuri, mapya na ya zamani, ambayo nimekuhifadhia wewe, mpenzi wangu.