Wimbo Ulio Bora 7:1-10
Wimbo Ulio Bora 7:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyayo zako katika viatu zapendeza sana! Ewe mwanamwali wa kifalme. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, kazi ya msanii hodari. Kitovu chako ni kama bakuli lisilokosa divai iliyokolezwa. Tumbo lako ni kama lundo la ngano lililozungushiwa yungiyungi kandokando. Matiti yako ni kama paa mapacha, ni kama swala wawili. Shingo yako ni kama mnara wa pembe za ndovu; macho yako ni kama vidimbwi mjini Heshboni, karibu na mlango wa Beth-rabi. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, ambao unauelekea mji wa Damasko. Kichwa chako juu yako ni kama mlima Karmeli, nywele zako za ukoka zangaa kama zambarau; uzuri wako waweza kumteka hata mfalme. Tazama ulivyo mzuri na wa kuvutia! Ewe mpenzi, mwali upendezaye! Umbo lako lapendeza kama mtende, matiti yako ni kama shada za tende. Nilisema nitaupanda mtende na kuzichuma shada za tende. Kwangu matiti yako ni kama shada za zabibu, harufu nzuri ya pumzi yako ni kama matofaa; na kinywa chako ni kama divai tamu. Basi divai na itiririke hadi kwa mpenzi wangu, ipite juu ya midomo yake na meno yake! Mimi ni wake mpenzi wangu, naye anionea sana shauku.
Wimbo Ulio Bora 7:1-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Binti wa kimalkia, jinsi ulivyo mzuri Hatua zako katika mitarawanda. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, Kazi ya mikono ya fundi stadi; Kitovu chako ni kama bakuli la mviringo, Na isikose divai iliyochanganyika; Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano, Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro; Matiti yako mawili ni kama wanapaa wawili, Ambao ni mapacha ya paa; Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe; Macho yako kama viziwa vya Heshboni, Karibu na mlango wa Beth-rabi; Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, Unaoelekea Dameski; Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli, Na nywele za kichwa chako kama urujuani, Mfalme amenaswa na mashungi yake. Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu, Mapenzi katikati ya anasa! Kimo chako kimefanana na mtende, Na matiti yako na vichala. Nilisema, Nitapanda huo mtende, Na kuyashika makuti yake. Matiti yako na yawe kama vichala vya mzabibu, Na harufu ya pumzi yako kama mapera; Na kinywa chako kama divai iliyo bora, Kwa mpendwa wangu inashuka taratibu, Ikitiririka midomoni mwao walalao. Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu.
Wimbo Ulio Bora 7:1-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Siti msharifu, jinsi zilivyo nzuri Hatua zako katika mitalawanda. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, Kazi ya mikono ya fundi mstadi; Kitovu chako ni kama bilauri iliyoviringana, Na isikose divai iliyochanganyika; Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano, Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro; Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili, Ambao ni mapacha ya paa; Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe; Macho yako kama viziwa vya Heshboni, Karibu na mlango wa Beth-rabi; Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, Unaoelekea Dameski; Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli, Na nywele za kichwa chako kama urujuani, Mfalme amenaswa na mashungu yake. Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu, Mapenzi katikati ya anasa! Kimo chako kimefanana na mtende, Na maziwa yako na vichala. Nilisema, Nitapanda huo mtende, Na kuyashika makuti yake. Maziwa yako na yawe kama vichala vya mzabibu, Na harufu ya pumzi yako kama mapera; Na kinywa chako kama divai iliyo bora, Kwa mpendwa wangu inashuka taratibu, Ikitiririka midomoni mwao walalao. Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu.
Wimbo Ulio Bora 7:1-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ee binti ya mwana wa mfalme, tazama jinsi inavyopendeza miguu yako katika viatu! Miguu yako yenye madaha ni kama vito vya thamani, kazi ya mikono ya fundi stadi. Kitovu chako ni kama bilauri ya mviringo ambayo kamwe haikosi divai iliyochanganywa. Kiuno chako ni kichuguu cha ngano kilichozungukwa kwa yungiyungi. Matiti yako ni kama wana-paa wawili, mapacha wa paa. Shingo yako ni kama mnara wa pembe ya ndovu. Macho yako ni vidimbwi vya Heshboni karibu na lango la Beth-Rabi. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni ukitazama kuelekea Dameski. Kichwa chako kinakuvika taji kama Mlima Karmeli. Nywele zako ni kama zulia la urujuani; mfalme ametekwa na mashungi yake. Tazama jinsi ulivyo mzuri na unavyopendeza, ee pendo, kwa uzuri wako! Umbo lako ni kama la mtende, nayo matiti yako kama vishada vya matunda. Nilisema, “Nitakwea mtende, nami nitayashika matunda yake.” Matiti yako na yawe kama vishada vya mzabibu, harufu nzuri ya pumzi yako kama matofaa, na kinywa chako kama divai bora kuliko zote. Divai na iende moja kwa moja hadi kwa mpenzi wangu, ikitiririka polepole juu ya midomo na meno. Mimi ni mali ya mpenzi wangu, nayo shauku yake ni juu yangu.