Wimbo Ulio Bora 6:4-13
Wimbo Ulio Bora 6:4-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Mpenzi wangu, wewe u mzuri kama Tirza, wapendeza kama Yerusalemu, unatisha kama jeshi lenye bendera. Hebu tazama kando tafadhali; ukinitazama nahangaika. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, wateremkao chini ya milima ya Gileadi. Meno yako kama kundi la kondoo majike wanaoteremka baada ya kuogeshwa. Kila mmoja amezaa mapacha, na hakuna yeyote aliyefiwa. Mashavu yako ni kama nusu mbili za komamanga, nyuma ya shela lako. Wapo malkia sitini, masuria themanini, na wasichana wasiohesabika! Hua wangu, mzuri wangu, ni mmoja tu, na ni kipenzi cha mama yake; yeye ni wa pekee kwa mama yake. Wasichana humtazama na kumwita heri, nao malkia na masuria huziimba sifa zake. Nani huyu atazamaye kama pambazuko? Mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua, na anatisha kama jeshi lenye bendera. Nimeingia katika bustani ya milozi kutazama machipuko ya bondeni, kuona kama mizabibu imechanua, na mikomamanga imechanua maua. Bila kutazamia, mpenzi wangu, akanitia katika gari la mkuu. Rudi, rudi ewe msichana wa Mshulami. Rudi, rudi tupate kukutazama.
Wimbo Ulio Bora 6:4-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mpenzi wangu, u mzuri kama Tirza, Mwenye kupendeza kama Yerusalemu, Wa kutisha kama jeshi lenye bendera. Uyageuzie macho yako mbali nami, Kwa maana yamenitisha sana. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, Wakijilaza mbavuni pa Gileadi. Meno yako kama kundi la kondoo, Wakipanda kutoka kuoshwa; Ambao kila mmoja amezaa mapacha, Wala hakuna aliyefiwa kati yao. Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga, Nyuma ya barakoa yako. Wako malkia sitini, na masuria themanini, Na wanawali wasiohesabika; Hua wangu, mkamilifu wangu, ni mmoja tu, Mtoto wa pekee wa mamaye. Ndiye kipenzi chake aliyemzaa, Binti wakamwona wakamwita heri; Malkia na masuria nao wakamwona, Wakamsifu, wakisema, Ni nani huyu atazamaye kama alfajiri, Mzuri kama mwezi, safi kama jua, Wa kutisha kama wenye bendera? Nilishukia katika bustani ya milozi, Ili kuyatazama machipuko ya bondeni; Nione kama mzabibu umechanua, Kama mikomamanga imetoa maua. Kabla sijajua, roho yangu ilinileta Katikati ya magari ya wakuu wangu. Rudi, rudi, Mshulami, Rudi, rudi, ili sisi tukutazame.
Wimbo Ulio Bora 6:4-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mpenzi wangu, u mzuri kama Tirza, Mwenye kupendeza kama Yerusalemu, Wa kutisha kama wenye bendera. Uyageuzie macho yako mbali nami, Kwa maana yamenitisha sana. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, Wakijilaza mbavuni pa Gileadi. Meno yako kama kundi la kondoo, Wakipanda kutoka kuoshwa; Ambao kila mmoja amezaa mapacha, Wala hakuna aliyefiwa kati yao. Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga, Nyuma ya barakoa yako. Wako malkia sitini, na masuria themanini, Na wanawali wasiohesabika; Hua wangu, mkamilifu wangu, ni mmoja tu, Mtoto wa pekee wa mamaye. Ndiye kipenzi chake aliyemzaa, Binti wakamwona wakamwita heri; Malkia na masuria nao wakamwona, Wakamsifu, wakisema, Ni nani huyu atazamaye kama alfajiri, Mzuri kama mwezi, safi kama jua, Wa kutisha kama wenye bendera? Nalishukia bustani ya milozi, Ili kuyatazama machipuko ya bondeni; Nione kama mzabibu umechanua, Kama mikomamanga imetoa maua. Kabla sijajua, roho yangu ilinileta Katikati ya magari ya wakuu wangu. Rudi, rudi, Mshulami, Rudi, rudi, ili sisi tukutazame.
Wimbo Ulio Bora 6:4-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wewe ni mzuri, mpendwa wangu, kama Tirsa, unapendeza kama Yerusalemu, umetukuka kama jeshi lenye bendera. Uyageuze macho yako mbali nami; yananigharikisha. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi wanaoteremka kutoka Gileadi. Meno yako ni kama kundi la kondoo wanaotoka kuogeshwa. Kila mmoja ana pacha lake, hakuna hata mmoja aliye peke yake. Mashavu yako nyuma ya shela yako ni kama vipande viwili vya komamanga. Panaweza kuwa na malkia sitini, masuria themanini, na mabikira wasiohesabika; lakini hua wangu, mkamilifu wangu, ni wa namna ya pekee, binti pekee kwa mama yake, kipenzi cha yeye aliyemzaa. Wanawali walimwona na kumwita aliyebarikiwa; malkia na masuria walimsifu. Ni nani huyu atokeaye kama mapambazuko, mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua, ametukuka kama nyota zinazofuatana? Niliteremka kwenye bustani ya miti ya milozi ili kutazama machipuko ya bondeni, kuona kama mizabibu imechipua au kama mikomamanga imechanua maua. Kabla sijangʼamua, shauku yangu iliniweka katikati ya magari ya vita ya wakuu wangu. Rudi, rudi, ee Mshulami; rudi, rudi ili tupate kukutazama!