Wimbo Ulio Bora 3:6-11
Wimbo Ulio Bora 3:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Ni kitu gani kile kitokacho jangwani kama mnara wa moshi, kinukiacho manemane na ubani, manukato yauzwayo na wafanyabiashara? Tazama! Ni machela ya Solomoni; amebebwa juu ya kiti chake cha enzi; amezungukwa na walinzi sitini, mashujaa bora wa Israeli. Kila mmoja wao ameshika upanga, kila mmoja wao ni hodari wa vita. Kila mmoja ana upanga wake mkononi, tayari kumkabili adui usiku. Mfalme Solomoni alijitengenezea machela, kwa mbao nzuri kutoka Lebanoni. Nguzo zake zilitengenezwa kwa fedha; mgongo wake kwa dhahabu; mahali pa kukalia pamefunikwa vitambaa vya zambarau, walichoshona kwa upendo wanawake wa Yerusalemu, waliokishonea alama za upendo. Njoni basi enyi wanawake wa Siyoni, mkamwone mfalme Solomoni. Amevalia taji aliyovikwa na mama yake, siku alipofanya harusi yake, naam, siku ambayo moyo wake ulijaa furaha.
Wimbo Ulio Bora 3:6-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi? Tazama, ni machela yake Sulemani; Mashujaa sitini waizunguka, Wa mashujaa wa Israeli. Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya kamsa za usiku. Mfalme Sulemani alijitengenezea machela Ya miti ya Lebanoni; Nguzo zake alizitengeneza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, Gari lake limenakishiwa njumu, Hiba ya binti za Yerusalemu. Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alilovikwa na mamaye, Siku ya posa yake, Siku ya furaha ya moyo wake.
Wimbo Ulio Bora 3:6-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi? Tazama, ni machela yake Sulemani; Mashujaa sitini waizunguka, Wa mashujaa wa Israeli. Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya kamsa za usiku. Mfalme Sulemani alijifanyizia machela Ya miti ya Lebanoni; Nguzo zake alizifanyiza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, Gari lake limenakishiwa njumu, Hiba ya binti za Yerusalemu. Tokeni, enyi binti za Sayuni, Mtazameni Mfalme Sulemani, Amevaa taji alivyovikwa na mamaye, Siku ya maposo yake, Siku ya furaha ya moyo wake.
Wimbo Ulio Bora 3:6-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwani kama nguzo ya moshi, anayenukia manemane na uvumba iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote vya mfanyabiashara? Tazama! Ni gari la Sulemani likisindikizwa na mashujaa sitini, walio wakuu sana wa Israeli, wote wamevaa panga, wote wazoefu katika vita, kila mmoja na upanga wake pajani, wamejiandaa kwa ajili ya vitisho vya usiku. Mfalme Sulemani alijitengenezea gari; alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni. Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha, kitako chake kwa dhahabu. Kiti chake kilipambwa kwa zambarau, gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo na binti za Yerusalemu. Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni, mkamtazame Mfalme Sulemani akiwa amevaa taji, taji ambalo mama yake alimvika siku ya arusi yake, siku ambayo moyo wake ulishangilia.