Wimbo Ulio Bora 3:1-5
Wimbo Ulio Bora 3:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Usiku nikiwa kitandani mwangu, niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu; nilimtafuta, lakini sikumpata. Niliamka nikazunguka mjini, barabarani na hata vichochoroni, nikimtafuta yule wangu wa moyo. Nilimtafuta, lakini sikumpata. Walinzi wa mji waliniona walipokuwa wanazunguka mjini. Basi nikawauliza, “Je, mmemwona mpenzi wangu wa moyo?” Mara tu nilipoachana nao, nilimwona mpenzi wangu wa moyo; nikamshika wala sikumwachia aondoke, hadi nilipompeleka nyumbani kwa mama yangu, hadi chumbani kwake yule aliyenizaa. Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu, kama walivyo paa au swala, msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi, hadi hapo wakati wake utakapofika.
Wimbo Ulio Bora 3:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usiku kitandani nilimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nilimtafuta, nisimpate. Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani, Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate. Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu? Kitambo kidogo tu nilipoachana nao, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa. Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
Wimbo Ulio Bora 3:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nalimtafuta, nisimpate. Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani, Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate. Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu? Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena, Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu, Chumbani mwake aliyenizaa. Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
Wimbo Ulio Bora 3:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usiku kucha kwenye kitanda changu nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata. Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini, katika barabara zake na viwanja; nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye. Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata. Walinzi walinikuta walipokuwa wakizunguka mji. Nikawauliza, “Je, mmemwona yule moyo wangu umpendaye?” Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita nilimpata yule moyo wangu umpendaye. Nilimshika na sikumwachia aende hadi nilipomleta katika nyumba ya mama yangu, katika chumba cha yule aliyenichukua mimba. Binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe.