Wimbo Ulio Bora 2:10-13
Wimbo Ulio Bora 2:10-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Mpenzi wangu aniambia: “Inuka basi, ewe mpenzi wangu, unipendezaye, njoo twende zetu. Tazama, majira ya baridi yamepita, nazo mvua zimekwisha koma; maua yamechanua kila mahali. Wakati wa kuimba umefika; sauti ya hua yasikika mashambani mwetu. Mitini imeanza kuzaa; na mizabibu imechanua; inatoa harufu nzuri. Njoo, basi, ewe mpenzi wangu unipendezaye, njoo twende.
Wimbo Ulio Bora 2:10-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako, Maana tazama, majira ya baridi yamepita, Masika imekwisha, imekwenda zake; Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kuimba umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu. Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
Wimbo Ulio Bora 2:10-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako, Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake; Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu. Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
Wimbo Ulio Bora 2:10-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia, “Inuka, mpendwa wangu, mrembo wangu, tufuatane. Tazama! Wakati wa masika umepita, mvua imekwisha na ikapita. Maua yanatokea juu ya nchi; majira ya kuimba yamewadia, sauti za njiwa zinasikika katika nchi yetu. Mtini unatunga matunda yake ya mwanzoni, zabibu zinazochanua zaeneza harufu nzuri. Inuka, njoo mpenzi wangu. Mrembo wangu, tufuatane.”