Wimbo Ulio Bora 2:1-6
Wimbo Ulio Bora 2:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi ni ua la Sharoni, ni yungiyungi ya bondeni. Kama yungiyungi kati ya michongoma, ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya wasichana. Kama mtofaa kati ya miti ya msituni, ndivyo alivyo mpenzi wangu kati ya wavulana. Nafurahia kuketi chini ya kivuli chake, na tunda lake tamu sana kwangu. Alinichukua hadi ukumbi wa karamu, akatweka bendera ya mapenzi juu yangu. Nishibishe na zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, maana naugua kwa mapenzi! Mkono wake wa kushoto chini ya kichwa changu, mkono wake wa kulia wanikumbatia.
Wimbo Ulio Bora 2:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi ni ua la uwandani, Ni fahirisi ya mabondeni. Kama fahirisi kati ya miiba, Kadhalika mpenzi wangu kati ya binti. Kama mpera kati ya miti ya msituni, Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana. Niliketi kivulini mwake kwa furaha, Na matunda yake niliyaonja kuwa matamu. Akanileta mpaka nyumba ya karamu, Na bendera yake juu yangu ni mapenzi. Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera, Kwa maana nimezimia kwa mapenzi. Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, Nao wa kulia unanikumbatia!
Wimbo Ulio Bora 2:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi ni ua la uwandani, Ni nyinyoro ya mabondeni. Kama nyinyoro kati ya miiba, Kadhalika mpenzi wangu kati ya binti. Kama mpera kati ya miti ya msituni, Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana. Naliketi kivulini mwake kwa furaha, Na matunda yake naliyaonja kuwa matamu. Akanileta mpaka nyumba ya karamu, Na bendera yake juu yangu ni mapenzi. Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera, Kwa maana nimezimia kwa mapenzi. Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, Nao wa kuume unanikumbatia!
Wimbo Ulio Bora 2:1-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mimi ni ua la Sharoni, yungiyungi ya bondeni. Kama yungiyungi kati ya miiba, ndivyo alivyo mpendwa wangu kati ya wanawali. Kama mti wa mtofaa miongoni mwa miti ya msituni, ndivyo alivyo mpenzi wangu miongoni mwa wanaume vijana. Ninafurahia kuketi kivulini mwa mwanaume huyu, na tunda lake ni tamu kwangu. Amenichukua hadi ukumbi wa karamu, na bendera ya huyu mwanaume juu yangu ni upendo. Nitie nguvu kwa zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, kwa maana ninazimia kwa mapenzi. Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kuume unanikumbatia.