Wimbo Ulio Bora 1:5-6
Wimbo Ulio Bora 1:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Enyi wanawake wa Yerusalemu, mimi ni mweusi na ninapendeza, kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya Solomoni. Msinishangae kwa sababu ni mweusi, maana jua limenichoma. Ndugu zangu walinikasirikia, wakanifanya mlinzi wa mashamba ya mizabibu. Lakini sikutunza shamba langu la mizabibu.
Wimbo Ulio Bora 1:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi ni mweusi mweusi, lakini napendeza, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
Wimbo Ulio Bora 1:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
Wimbo Ulio Bora 1:5-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Sulemani. Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. Wana wa mama yangu walinikasirikia na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.