Wimbo Ulio Bora 1:3-4
Wimbo Ulio Bora 1:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Manukato yako yanukia vizuri, na jina lako ni kama marashi yaliyomiminwa. Kwa hiyo wanawake hukupenda! Nichukue, twende zetu haraka, mfalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wanawake wana haki kukupenda!
Wimbo Ulio Bora 1:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda. Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutalinena pendo lako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.
Wimbo Ulio Bora 1:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda. Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutazinena pambaja zako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.