Wimbo Ulio Bora 1:1-6
Wimbo Ulio Bora 1:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Wimbo wa Solomoni ulio bora kuliko nyimbo zote. Heri midomo yako inibusu, maana pendo lako ni bora kuliko divai. Manukato yako yanukia vizuri, na jina lako ni kama marashi yaliyomiminwa. Kwa hiyo wanawake hukupenda! Nichukue, twende zetu haraka, mfalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wanawake wana haki kukupenda! Enyi wanawake wa Yerusalemu, mimi ni mweusi na ninapendeza, kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya Solomoni. Msinishangae kwa sababu ni mweusi, maana jua limenichoma. Ndugu zangu walinikasirikia, wakanifanya mlinzi wa mashamba ya mizabibu. Lakini sikutunza shamba langu la mizabibu.
Wimbo Ulio Bora 1:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wimbo ulio bora, wa Sulemani. Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pendo lako lapita divai; Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda. Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutalinena pendo lako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende. Mimi ni mweusi mweusi, lakini napendeza, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
Wimbo Ulio Bora 1:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wimbo ulio bora, wa Sulemani. Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zako zapita divai; Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda. Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutazinena pambaja zako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende. Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
Wimbo Ulio Bora 1:1-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wimbo ulio bora wa Sulemani. Unibusu kwa busu la kinywa chako, kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai. Manukato yako yananukia vizuri, jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. Ndiyo sababu wanawali wanakupenda! Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako kuliko divai. Tazama jinsi ilivyo bora wakupende! Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Sulemani. Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. Wana wa mama yangu walinikasirikia na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.