Wimbo Ulio Bora 1:1-11
Wimbo Ulio Bora 1:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Wimbo wa Solomoni ulio bora kuliko nyimbo zote. Heri midomo yako inibusu, maana pendo lako ni bora kuliko divai. Manukato yako yanukia vizuri, na jina lako ni kama marashi yaliyomiminwa. Kwa hiyo wanawake hukupenda! Nichukue, twende zetu haraka, mfalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kushangilia kwa sababu yako, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wanawake wana haki kukupenda! Enyi wanawake wa Yerusalemu, mimi ni mweusi na ninapendeza, kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya Solomoni. Msinishangae kwa sababu ni mweusi, maana jua limenichoma. Ndugu zangu walinikasirikia, wakanifanya mlinzi wa mashamba ya mizabibu. Lakini sikutunza shamba langu la mizabibu. Hebu niambie ee wangu wa moyo, utawalisha wapi kondoo wako? Ni wapi watakapopumzikia adhuhuri? Kwa nini mimi nikutafute kati ya makundi ya wenzako? Ewe upendezaye kuliko wanawake wote; kama hujui, fanya hivi: Zifuate nyayo za kondoo; basi, walishe mbuzi wako karibu na hema za wachungaji. Wewe ee mpenzi wangu, nakulinganisha na farasi dume wa magari ya Farao. Mashavu yako yavutia kwa vipuli, na shingo yako kwa mikufu ya johari. Lakini tutakufanyizia mikufu ya dhahabu, iliyopambwa barabara kwa fedha.
Wimbo Ulio Bora 1:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wimbo ulio bora, wa Sulemani. Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pendo lako lapita divai; Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda. Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutalinena pendo lako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende. Mimi ni mweusi mweusi, lakini napendeza, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda. Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa shela, Karibu na makundi ya wenzako? Usipojua, wewe uliye mzuri katika wanawake, Shika njia uzifuate nyayo za kondoo, Na kuwalisha wana-mbuzi wako Karibu na hema za wachungaji. Mpenzi wangu, nimekulinganisha Na farasi katika magari ya Farao. Mashavu yako ni mazuri kwa mashada, Shingo yako kwa mikufu ya vito. Tutakutengenezea mashada ya dhahabu, Yenye vifungo vya fedha.
Wimbo Ulio Bora 1:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wimbo ulio bora, wa Sulemani. Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zako zapita divai; Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda. Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutazinena pambaja zako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende. Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda. Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa kidoto, Karibu na makundi ya wenzako? Usipojua, wewe uliye mzuri katika wanawake, Shika njia uzifuate nyayo za kondoo, Na kuwalisha wana-mbuzi wako Karibu na hema za wachungaji. Mpenzi wangu, nimekulinganisha Na farasi katika magari ya Farao. Mashavu yako ni mazuri kwa mashada, Shingo yako kwa mikufu ya vito. Tutakufanyizia mashada ya dhahabu, Yenye vifungo vya fedha.
Wimbo Ulio Bora 1:1-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wimbo ulio bora wa Sulemani. Unibusu kwa busu la kinywa chako, kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai. Manukato yako yananukia vizuri, jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. Ndiyo sababu wanawali wanakupenda! Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako kuliko divai. Tazama jinsi ilivyo bora wakupende! Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Sulemani. Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. Wana wa mama yangu walinikasirikia na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha. Niambie, wewe ninayekupenda, unalisha wapi kundi lako la kondoo na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri. Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela karibu na makundi ya rafiki zako? Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote, fuata nyayo za kondoo, na kulisha wana-mbuzi wako karibu na mahema ya wachungaji. Mpendwa wangu, ninakufananisha na farasi jike aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao. Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli, shingo yako ikiwa na mikufu ya vito. Tutakufanyia vipuli vya dhahabu, vyenye kupambwa kwa fedha.