Ruthu 4:16-21
Ruthu 4:16-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi Naomi alimchukua mtoto huyo akamweka kifuani mwake na kumlea. Wanawake majirani walimwita mtoto huyo Obedi wakisema, “Mtoto amezaliwa kwa Naomi.” Hatimaye Obedi akamzaa Yese aliyemzaa Daudi. Na hivi ndivyo vizazi vya Peresi: Peresi alimzaa Hesroni, Hesroni akamzaa Rami, Rami akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nahshoni, Nahshoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi, Boazi akamzaa Obedi
Ruthu 4:16-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake. Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi. Hivi ndivyo vizazi vya Peresi; Peresi alimzaa Hesroni; na Hesroni akamzaa Ramu; na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni; na Nashoni akamzaa Salmoni; na Salmoni akamzaa Boazi; na Boazi akamzaa Obedi
Ruthu 4:16-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake. Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi. Hivi ndivyo vizazi vya Peresi; Peresi alimzaa Hesroni; na Hesroni akamzaa Ramu; na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni; na Nashoni akamzaa Salmoni; na Salmoni akamzaa Boazi; na Boazi akamzaa Obedi
Ruthu 4:16-21 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Basi Naomi akamchukua yule mtoto, akampakata na akawa mlezi wake. Wanawake waliokuwa jirani zake wakasema, “Naomi ana mtoto wa kiume.” Wakamwita jina Obedi. Yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi. Hivi ndivyo vizazi vya Peresi: Peresi alimzaa Hesroni, Hesroni akamzaa Ramu, Ramu akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nashoni, Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi, Boazi akamzaa Obedi