Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ruthu 4:1-8

Ruthu 4:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

Boazi alikwenda mahali pa kufanyia mkutano huko kwenye lango la mji akaketi chini. Kisha yule ndugu ya Elimeleki ambaye Boazi alikuwa amemtaja, akapita karibu na hapo. Boazi akamwita, akasema, “Njoo, uketi hapa ndugu.” Basi huyo mtu akaja na kuketi hapo. Ndipo Boazi akawaita wazee kumi wa mji, akawaomba wao pia waketi hapo. Wakaketi. Ndipo Boazi akamwambia yule ndugu yake, “Sasa Naomi ambaye amerudi kutoka Moabu, anataka kuliuza shamba ambalo lilikuwa la jamaa yetu Elimeleki. Basi mimi nimeona afadhali nikujulishe habari hii. Sasa ikiwa unalitaka shamba hili, toa fidia ulichukue mbele ya wazee wa watu wangu. Ikiwa unalitaka au hulitaki sema basi kwa kuwa nafasi ya kwanza ya kulifidia ni yako na yangu ni ya pili.” Naye akasema, “Mimi nitalifidia.” Boazi akasema, “Ni vyema, lakini ukilichukua hilo shamba kutoka kwa Naomi, basi utakuwa unamchukua pia Ruthu Mmoabu, mjane ambaye ni jamaa ya marehemu ili kwamba shamba hilo libaki katika jamaa ya huyo marehemu.” Yule jamaa aliyekuwa wa karibu akajibu, “Ikiwa ni hivyo, sitalifidia shamba hilo, kwa sababu yaonekana kuwa nitauharibu urithi wangu. Afadhali haki yangu ya kulichukua nikupe wewe, maana mimi siwezi kulifidia.” Siku zile, katika Israeli ikiwa watu walitaka kukomboa au kubadilishana kitu, ilikuwa ni desturi kwa mtu kuonesha ishara kwa kuvua kiatu chake na kumpa mwingine. Kwa ishara hiyo Waisraeli walionesha kwamba mambo yamesawazishwa. Basi, mtu huyo alimwambia Boazi, “Lifidie shamba,” kisha alivua kiatu chake na kumpa.

Shirikisha
Soma Ruthu 4

Ruthu 4:1-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Boazi akakwea hadi lango la mji, akaketi pale. Yule mtu wa jamaa aliyekuwa wa karibu wa kukomboa, ambaye Boazi alimtaja, akaja. Boazi akasema, “Njoo hapa, rafiki yangu. Karibu uketi.” Naye akakaribia, akaketi. Boazi akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, “Ketini hapa.” Nao wakaketi. Kisha akamwambia yule jamaa wa karibu wa kukomboa, “Naomi, aliyerudi hapa kutoka nchi ya Moabu, anauza sehemu ya ardhi iliyokuwa mali ya ndugu yetu Elimeleki. Nami niliwaza nikujulishe wewe na kukuambia uinunue mbele ya hawa waliopo hapa, na mbele ya wazee wa watu wangu. Kama wewe utaikomboa, haya fanya hivyo. Lakini kama hutaikomboa, uniambie, ili nijue. Kwa kuwa hakuna mtu mwingine mwenye haki ya kuikomboa ila wewe na baada yako ni mimi.” Naye akasema, “Nitaikomboa mimi.” Ndipo Boazi akasema “Siku utakaponunua hiyo ardhi kutoka kwa Naomi na Ruthu, Mmoabu, itakubidi kumchukua pia huyo mjane, ili kudumisha jina la marehemu pamoja na mali yake.” Aliposikia hili, yule jamaa wa karibu wa kukomboa akasema, “Basi mimi sitaweza kuikomboa, kwa sababu inaonekana nitauhatarisha urithi wangu. Wewe ikomboe mwenyewe. Mimi sitaweza.” (Basi katika siku za kale huko Israeli, ili kukamilisha tendo la kukomboa na kukabidhiana mali, mmoja huvua kiatu chake na kumpatia mwingine. Hii ilikuwa ni njia ya kuhalalisha mabadilishano katika Israeli.) Basi yule jamaa wa karibu wa kukomboa akamwambia Boazi, “Wewe inunue mwenyewe.” Naye huyo jamaa akavua kiatu chake.

Shirikisha
Soma Ruthu 4