Ruthu 3:16-18
Ruthu 3:16-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Alipofika mjini, mkwewe akamwuliza, “Ilikuwaje binti yangu?” Ruthu akamweleza yote ambayo Boazi alimtendea. Halafu akaendelea kusema, “Aliniambia nisirudi nyumbani kwa mkwe wangu mikono mitupu na kwa hiyo alinipa shayiri hii ipatayo vipimo sita.” Naye Naomi akasema, “Sasa tulia binti yangu Ruthu, mpaka uone litakalotokea. Boazi hatatulia leo mpaka ameyatimiza yote.”
Ruthu 3:16-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi alipofika kwa mkwewe, huyo akamwuliza, Je! Mwanangu, imekuwaje? Akamwambia yote yule mtu aliyomfanyia. Akasema, Na vipimo hivi sita vya shayiri amenipa; maana aliniambia, Usiende kwa mkweo mikono mitupu. Naye mkwewe akasema, Basi, mwanangu, tulia; hadi utakapojua jinsi litakavyotukia jambo hili; kwa sababu mtu huyu hataridhika, asipolimaliza jambo hilo leo.
Ruthu 3:16-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi alipofika kwa mkwewe, huyo akamwuliza, Je! Mwanangu, imekuwaje? Akamwambia yote yule mtu aliyomfanyia. Akasema, Na vipimo hivi sita vya shayiri amenipa; maana akaniambia, Usiende kwa mkweo mikono mitupu. Naye mkwewe akasema, Basi, mwanangu, tulia; hata utakapojua jinsi litakavyotukia jambo hili; kwa sababu mtu huyu hataridhika, asipolimaliza jambo hilo leo.
Ruthu 3:16-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Basi Ruthu alipofika kwa mama mkwe wake Naomi, akamuuliza, “Je, binti yangu, ilikuwaje huko?” Ndipo akamwelezea kila kitu Boazi alichomfanyia. Akaendelea kusema, “Amenipa shayiri vipimo sita, akaniambia, ‘Usiende kwa mama mkwe wako mikono mitupu.’ ” Kisha Naomi akasema, “Subiri binti yangu, hadi utakapojua kwamba hili jambo limeendaje. Kwa sababu mtu huyu hatatulia hadi akamilishe jambo hili leo.”