Ruthu 2:15-17
Ruthu 2:15-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Na ikawa Ruthu alipoendelea kuokota mavuno, Boazi aliwaambia wafanyakazi wake, “Mwacheni akusanye hata mahali miganda ilipo wala msimkemee. Zaidi ya hapo, vuteni masuke kutoka katika matita na mumwachie aokote bila kumkaripia.” Basi Ruthu aliendelea kuokota masuke mpaka jioni; na baada ya kupura hiyo shayiri alipata debe moja na zaidi.
Ruthu 2:15-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye alipoinuka tena ili aende kuokota masazo, huyo Boazi aliwaagiza vijana wake akisema, Mwacheni aokote hata kati ya miganda, wala msimkemee. Tena mtoleeni kidogo katika matita na kukiacha, na akiokote, wala msimkataze. Basi Ruthu akaokota mabaki shambani hadi jioni; kisha akazipura zile nafaka alizoziokota, zikawa yapata efa moja ya shayiri.
Ruthu 2:15-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye alipoinuka tena ili aende kuokota masazo, huyo Boazi aliwaagiza vijana wake akisema, Mwacheni aokote hata kati ya miganda, wala msimkemee. Tena mtoleeni kidogo katika matita na kukiacha, na akiokote, wala msimkataze. Basi Ruthu akaokota masazo kondeni hata jioni; kisha akazipura zile nafaka alizoziokota, zikawa yapata efa moja ya shayiri.
Ruthu 2:15-17 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Alipoinuka ili kuokota mabaki ya nafaka, Boazi akawaagiza watu wake, “Hata kama atakusanya kati ya miganda, msimzuie. Badala yake, toeni masuke katika miganda, mwachieni ayaokote, na msimkemee.” Basi Ruthu akaokota masazo shambani hata jioni. Akatwanga ile shayiri aliyokusanya, ikajaa efa moja.