Ufunuo 8:13
Ufunuo 8:13 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha, nikatazama, nikasikia tai akiruka juu kabisa angani, anasema kwa sauti kubwa, “Ole, ole, ole kwa wanaoishi duniani wakati malaika watatu waliobaki watakapopiga tarumbeta zao!”
Ufunuo 8:13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti za baragumu ziliobakia za malaika watatu, walio tayari kupiga.
Ufunuo 8:13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga.
Ufunuo 8:13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nilipokuwa tena nikitazama, nikamsikia tai mmoja akipaza sauti kwa nguvu, huku akiruka katikati ya anga, akasema, “Ole! Ole! Ole wa watu wanaoishi duniani, kwa sababu ya tarumbeta ambazo malaika hao wengine watatu wanakaribia kuzipiga!”