Ufunuo 7:7-9
Ufunuo 7:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
kabila la Simeoni, 12,000; kabila la Lawi, 12,000; kabila la Isakari, 12,000; kabila la Zebuluni, 12,000; kabila la Yosefu, 12,000; na kabila la Benyamini, 12,000. Kisha, nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu wasiohesabika: Watu wa kila taifa, ukoo, jamaa na lugha. Nao walikuwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo, wamevaa mavazi meupe na kushika matawi ya mitende mikononi mwao.
Ufunuo 7:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wa kabila la Simeoni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Lawi elfu kumi na mbili. Wa kabila la Isakari elfu kumi na mbili. Wa kabila la Zabuloni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Yusufu elfu kumi na mbili. Wa kabila la Benyamini elfu kumi na mbili waliotiwa mhuri. Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao
Ufunuo 7:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao
Ufunuo 7:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
kutoka kabila la Simeoni elfu kumi na mbili, kutoka kabila la Lawi elfu kumi na mbili, kutoka kabila la Isakari elfu kumi na mbili, kutoka kabila la Zabuloni elfu kumi na mbili, kutoka kabila la Yusufu elfu kumi na mbili, na kutoka kabila la Benyamini elfu kumi na mbili. Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuwahesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao.