Ufunuo 2:2-4
Ufunuo 2:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Najua mambo yako yote; najua bidii yako na uvumilivu wako. Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume na kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo. Wewe unayo saburi, umestahimili taabu nyingi kwa ajili ya jina langu, wala hukuvunjika moyo. Lakini ninalo jambo moja dhidi yako: Wewe hunipendi tena sasa kama pale awali.
Ufunuo 2:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ninayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wanaojiita mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.
Ufunuo 2:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.
Ufunuo 2:2-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewajaribu wale wanaojifanya mitume na kumbe sio, nawe umewatambua kuwa ni waongo. Umevumilia na kustahimili taabu kwa ajili ya Jina langu, wala hukuchoka. Lakini nina neno dhidi yako: Umeuacha upendo wako wa kwanza.