Ufunuo 14:3-4
Ufunuo 14:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Walikuwa wanaimba wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi na mbele ya wale viumbe hai wanne na wale wazee. Hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao watu 144,000 waliokombolewa duniani. Watu hao ndio wale ambao hawakujichafua na wanawake, nao ni mabikira. Wao humfuata Mwanakondoo kokote aendako. Wamekombolewa kutoka miongoni mwa binadamu wengine, wakawa wa kwanza kutolewa kwa Mungu na kwa Mwanakondoo.
Ufunuo 14:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hakuna mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale elfu mia moja na arubaini na nne, walionunuliwa katika nchi. Hawa ndio wasiojitia unajisi na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-kondoo.
Ufunuo 14:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi. Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.
Ufunuo 14:3-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nao wakaimba wimbo mpya mbele ya hicho kiti cha enzi, na mbele ya wale viumbe wanne wenye uhai, na wale wazee. Hakuna mtu yeyote aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao elfu mia moja na arobaini na nne waliokuwa wamekombolewa kutoka duniani. Hawa ndio wale ambao hawakujitia unajisi kwa wanawake, kwa kuwa wao ni bikira. Wao humfuata Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamekombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu wakawa malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.